Na mwandishi wetu,Mpwapwa.
MWALIMU wa shule ya Msingi Kisokwe, Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma Albert Kaguli (43) amekutwa ameuawa na watu wasio julikana kwa kupigwa kichwani na kitu kinachosadikiwa kuwa kizito.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP)Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini aliyefanya uhalifu huo.
Aidha amesema jeshi hilo pia linamtafuta mtu mmoja anaye julikana kwa jina la Shukuran Maselo Kwa uchunguzi zaidi kwa kushukiwa kushiriki katika mauaji hayo ambayo chanzo chake inadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kutokana na tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Josephat Maganga amelaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkoni.