Mahakama ya Makadara
**
Mahakama ya Makadara nchini Kenya, imemhukumu kifungo cha miezi nane gerezani, mwanamke mmoja aitwaye Mary Ambeza, kwa kosa la kujiteka nyara na kumtumia ujumbe mume wake uliosema, “Njoo uchukue mwili wa mkeo”
Mary Ambeza alihukumiwa kifungo hicho baada ya kukiri kosa la kujiteka nyara mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo Hellen Onkwany.
Taarifa zinaeleza kuwa Ambeza alitoweka Februari 7 mwaka huu baada ya kuondoka nyumbani kwake kuelekea kazini kabla ya kumtumia mumewe Dominic Oduor Otieno ujumbe mfupi akimjulisha kuwa alikuwa ametekwa nyara na watu wasiojulikana.
"Otieno alipata ujumbe kupitia nambari ya simu ya mkewe majira ya saa 3:00 usiku uliosema, njoo uchukue mwili wa mkeo," Mwendesha mashtaka aliiambia Mahakama.
Ambapo Otieno mara baada ya kupokea ujumbe huo wa kutia wasiwasi, alienda kituo cha polisi cha Dandoraeneo la Kamkunji Jjijini Nairobi kutoa taarifa ya kupotea kwa mke wake na baada ya uchunguzi polisi ulibaini kwamba mwanamke huyo alighushi utekaji nyara wake.
Social Plugin