Madereva wa pikipiki maarufu bodaboda kwa kushirikiana na polisi katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, wameupata mwili wa kijana Mohamed Juma (22) akiwa amefariki dunia katika pori la Kijiji cha Hiari, wilayani Mtwara.
Inadaiwa kuwa siku sita zilizopita, kijana huyo alikodishwa usafiri huo na watu wawili ambao hawajafahamika hadi sasa, wakitaka awapeleke kijijini hapo, na kijana huyo hakuonekana tena hadi mwili wake ulipokutwa leo porini humo ukiwa umefungwa kamba na ukiwa na majeraha.
Social Plugin