Baada ya kutangaza mashambulizi dhidi ya Ukraine, Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametoa onyo kwa Mataifa ya Magharibi kuingilia kinachoendelea baina ya Nchi hizo.
Mara baada ya milipuko kuripotiwa katika Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv Putin alinukuliwa akisema, “Kwa yeyote atakayeingilia kutoka nje, atakutana na matokeo ambayo hajakutana nayo katika historia…”
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliitisha Kikao cha Dharura mara baada ya Urusi kuanza mashambulizi.
Hatua ya Urusi kuvamia Ukraine imeathiri usafiri wa angani barani Ulaya huku mashirika ya ndege yakiepuka anga ya Ukraine wakati mzozo wake na Urusi ukizidi kufukuta.
Ukraine ilifunga anga yake kwa safari za ndege za kiraia saa za mapema baada ya Urusi kuanza mashambulizi yake.
Waziri wa Uchukuzi wa Uingereza Grant Shapps ameagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga kuhakikisha mashirika ya ndege yanaepuka anga ya Ukraine "kufuatia matukio ya kutisha usiku mmoja".
Social Plugin