Mwakilishi wa Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Uvuvi, Bw. Amos Machilika (aliyesimama) akifungua Warsha ya kutambulisha Mradi wa Kupunguza Umasikini na Kuongeza Usalama wa Chakula na Lishe kwa wavuvi wadogo unaozingatia usawa wa kijinsia ambapo amesema kuwa Wizara imeandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutekeleza Mwongozo wa Hiari. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Dkt. Oliva Mkumbo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uvuvi, Bw. Didas Mtambalike, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi, Bi. Fatma Sobo na Mwakilishi wa Jukwaa la Wanawake (TAWFA). Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel Manispaa ya Morogoro.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uvuvi, Bw. Didas Mtambalike (aliyesimama) akizungumza kabla ya kufunguliwa kwa Warsha ya kutambulisha Mradi wa Kupunguza Umasikini na Kuongeza Usalama wa Chakula na Lishe kwa wavuvi wadogo unaozingatia usawa wa kijinsia. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel Manispaa ya Morogoro.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Dkt. Oliva Mkumbo (kushoto) akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa Warsha ya kutambulisha Mradi wa Kupunguza Umasikini na Kuongeza Usalama wa Chakula na Lishe kwa wavuvi wadogo unaozingatia usawa wa kijinsia. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel Manispaa ya Morogoro.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi, Bi. Fatma Sobo (aliyesimama) akitoa maelezo mafupi kuhusu mradi wakati wa Warsha ya kutambulisha Mradi wa Kupunguza Umasikini na Kuongeza Usalama wa Chakula na Lishe kwa wavuvi wadogo unaozingatia usawa wa kijinsia. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel Manispaa ya Morogoro.
Mwakilishi wa Jukwaa la Wanawake (TAWFA), Beatrice Mbaga (kulia) akitoa salam wakati wa Warsha ya kutambulisha Mradi wa Kupunguza Umasikini na Kuongeza Usalama wa Chakula na Lishe kwa wavuvi wadogo unaozingatia usawa wa kijinsia. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel Manispaa ya Morogoro.
Afisa Uvuvi Mwandamizi, Bi. Upendo Hamidu akiwasilisha mada kwenye Warsha ya kutambulisha Mradi wa Kupunguza Umasikini na Kuongeza Usalama wa Chakula na Lishe kwa wavuvi wadogo unaozingatia usawa wa kijinsia. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel Manispaa ya Morogoro.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi, Bw. Amos Machilika (kushoto) akikabidhi vitabu vya Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu kwa baadhi ya washiriki wa Washiriki wa warsha ya kutambulisha Mradi wa Kupunguza Umasikini na Kuongeza Usalama wa Chakula na Lishe kwa wavuvi wadogo unaozingatia usawa wa kijinsia. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel Manispaa ya Morogoro.
Picha ya pamoja ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi, Bw. Amos Machilika (katikati waliokaa) na Washiriki wa warsha ya kutambulisha Mradi wa Kupunguza Umasikini na Kuongeza Usalama wa Chakula na Lishe kwa wavuvi wadogo unaozingatia usawa wa kijinsia. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel Manispaa ya Morogoro.
.... ..........................................
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Uvuvi imeendelea kuwajali wavuvi wadogo kwa kuanzisha mradi wa kupunguza umasikini na kuongeza usalama wa chakula na lishe unaozingatia usawa wa kijinsia.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Amos Machilika wakati akifungua Warsha ambayo imewashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika taasisi za serikali, mashirika binafsi, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na baadhi ya Halmashauri zenye shughuli za uvuvi. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hotel ya Edema Manispaa ya Morogoro.
Bw. Machilika amesema kuwa katika kutekeleza Mwongozo wa Hiari wa kuendeleza uvuvi mdogo, Wizara imeandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutekeleza mwongozo huo ambao ulipitishwa na wadau wote na sasa unakwenda kutekelezwa.
Lengo la kuwa na warsha hiyo ya wadau ni kuwakutanisha wadau na kuwafahamisha kuhusu utekelezaji wa mpango wa huo wa kitaifa, pia kutambulisha mradi utakaotekeleza mpango kazi wa kitaifa. Kupitia mradi huo serikali inatarajia jamii hasa za wavuvi kupunguza umaskini, kuboresha lishe na kuongeza kipato kupitia shughuli zinazofanyika kutokana na mnyororo wa thamani wa mazao yatokanayo na uvuvi mdogo. Vilevile katika Warsha hiyo washiriki watafahamishwa kuhusu maadhimisho ya mwaka ya kitaifa ya uvuvi mdogo na ukuzaji viumbe maji wa mwaka huu 2022. Mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka miwili.
Naye mwakilishi wa FAO kwa upande wa sekta ya uvuvi, Dkt. Oliva Mkumbo amesema kuwa Tanzania ndio nchi ya kwanza kuandaa Mpango kazi wa kitaifa wa kutekeleza mwongozo wa hiari. Pia ameipongeza serikali kwa kuendelea kuwajali akina mama wanaojishughulisha na uvuvi mdogo ikiwa ni pamoja na Jukwaa la Wanawake (TAWFA)
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uvuvi, Didas Mtambalike amesema kuwa mradi huu utaanza kutekelezwa katika Halmashauri tano za Kilwa, Pangani, Mwanga, Kigoma na Ilemela. Vilevile amesema kuwa Wizara imefanikiwa kuanzisha jukwaa la wanawake wanaojishughulisha na uvuvi, kuandaa mpango kazi wa utekelezaji mwongozo wa hiari, kuandaa mradi huo kwa kushirikiana na FAO na kuanzisha dawati la jinsia wizarani linalosimamiwa na mvuvi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi, Bi. Fatma Sobo ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwajali wavuvi wadogo hasa kwa kuzingatia jinsia. Pia amepongeza uanzishwaji wa mradi huo kwa kuwa utasaidia sana katika kupunguza umasikini, kuwa na uhakika wa chakula na lishe bora, pamoja na kuwaongezea kipato wavuvi wadogo.