Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : ALLY SONSO AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa mchezaji wa Ruvu Shooting, Ally Mtoni “Sonso” (29) amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa Matibabu leo Ijumaa, Februari 11, 2022.

Taarifa za awali zinasema kuwa, Sonso ambaye alikuwa beki wa kushoto alikuwa akiugua maradhi ya muda mrefu. Kwa nyakati tofauti, Sonso amezitumika timu za Lipuli FC, Yanga SC, Kagera Sugar, Polisi Tanzania. Pia amewahi kucheza timu ya Taifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com