MKOA WA DODOMA KUSOMESHA WANAFUNZI WENYE UFAULU DARAJA LA KWANZA


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka, akimkabidhi cheti pamoja na Madaftari Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato,Anthia Kachelenesa kwa kufanya vizuri katika mtihani wa Kidato cha nne (CSEE) 2021 na kupata ufaulu wa Daraja la Kwanza kwa Tarakimu 1 (Single digit) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma. Picha na Alex Sonna.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka, akimkabidhi cheti Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mpwapwa Hildagarda Remy kutambua jitihada na umahiri wake katika ufundishaji wa somo la lake na kuwezesha wanafunzi zaidi ya kumi kufaulu kwa daraja ”A” katika mtihani wao wa kidato cha nne 2021 (CSEE) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma. Picha na Alex Sonna

 Na Dotto Kwilasa, Malunde 1 Blog-DODOMA.

SERIKALI  Mkoani Dodoma imesema imeweka mkakati wa kuwasomesha wanafunzi 43 kidato cha tano na sita waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne 2021 kwa shule za serikali za sekondari zilizopo Jijini Dodoma.

Kati ya wanafunzi hao wanaotarajiwa kusomeshwa ni wasichana 35 wakati wavulana ni  8  wenye ufaulu wa  daraja la kwanza alama 7 na wasichana wenye ufaulu wa daraja la kwanza  alama 7 hadi 9.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka katika hafla ya utoaji tuzo  kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne  mwaka 2021,huku akisema watagharamia vifaa vya shule pamoja na kulipa kwa kipindi cha miaka miwili.

Katika kuwapa motisha walimu ,Mkuu  huyo wa Mkoa  amenunua alama "A" kwa shilingi 5000 kwa walimu wa shule za sekondari waliowasaidia wanafunzi kupata alama hizo huku akidai kwa mwaka 2022 atanunua kwa Shilingi 10,000.

"Tunataka kuwa na alama nzuri kwenye huu mkoa,tunawapa motisha walimu wa masomo ambayo wamepata alama hiyo na kila mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza ,lazima Kila mmoja asimame kwenye nafasi yake kutimiza majukumu,"amesema.

Amesema ,Serikali inataka kuona walimu na wanafunzi kwa pamoja wanakuwa na ushindani kwenye uchumi hivyo lazima wawekeze katika suala la  elimu kwani hakuna nchi duniani iliyoendelea bila kuwekeza katika elimu.

Wanafunzi wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk. Fatuma Mganga,akielezea mikakati ya mkoa huo katika suala la elimu wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri,akielezea mikakati ya wilaya yake katika kutoa elimu pamoja na ufaulu wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Viongozi mbalimbali na walimu wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2021 .


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post