Waandishi wawili wa habari mkoani Arusha, Victor Korumba Moshi wa Global TV na Alphonce Kusaga wa Redio Triple A wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo katika kituo cha Polisi Azimio.
Waandishi hao wamekamatwa leo Alhamisi, Februari 24, 2022 wakati wakiwa katika kutimiza majukumu yao ya habari.
Taarifa za kukamatwa kwa waandishi wa Habari jijini Arusha
Waandishi wawili Victor Korumba wa Global Tv na Alphonce Kusaga wa Triple A FM wanashikiliwa na polisi kituo kikuu, walikuwa wakifuatilia tukio la askari kituo cha polisi sakina kupiga raia jana feb23, 2022.
Nimeongea na Mwenyekiti wa Arusha Press Club amethibitisha na sasa yupo kituo cha Polisi kufuatilia tukio hilo.
Tunaendelea kufuatilia tukio hilo.
Edwin Soko
24.02.2022
Social Plugin