WANAUME kutoka Kijiji cha Kagumoini, eneo bunge la Gatundu Kusini, kaunti ya Kiambu nchini Kenya wamelalamikia wakidai kuwa wake zao ni wachafu kupindukia.
Wanaume hao wanalalamika kuwa wake zao wanashindwa hata kubadilisha nguo kwa zaidi ya wiki moja, hali ambayo inachochea ndoa nyingi kuvunjika.
Hali hiyo wanadai kuwa imechangiwa na uhaba wa maji katika kijiji hicho kutokana na mtoa huduma ya maji wa eneo hilo kuacha kuvuta maji hadi majumbani mwao.
“Wake zetu ndio wanateseka zaidi kwani wanaishi na nguo moja kwa wiki nzima bila kubadilisha. Harufu inayotoka katika nyumba mbalimbali haiwezi kuvumilika tena,” Elijah Mungai Mumu, mkazi wa eneo hilo alisema.
Kutokana na changamoto hiyo ya zaidi ya miaka miwili, wanawake wa kijiji hicho wanalazimika kusafiri zaidi ya kilomita mbili kutafuta maji katika mto Rwabura.
Wanawake wasema nini?
Katika kujibu malalamiko ya waume zao, wanawake hao walimuomba Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati suala hilo kabla ya hajaondoka madarakani wakidai wametishiwa kuachwa na waume zao.
“Hakika tunapaswa kusikilizwa ikiwa familia zetu zitasimama. Tumeachana na ufugaji kwani hatuwezi kulisha mifugo kwa maji ya kutosha. Tunamwomba Rais Uhuru Kenyatta aingilie kati kabla hajastaafu,” Hellen Mwangi, mkazi mwingine alisema.
Social Plugin