Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WASAFI WAMPA DKT.ABBASI KEKI YA BIRTHDAY,USIKU WA WAPENDANAO


***************

Na. John Mapepele

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amepamba hafla ya Usiku wa Mahaba ndi ndi ndi baada ya kuandaliwa keki maalum ya siku yake ya kuzaliwa na kuimbiwa wimbo wa kuzaliwa ulioongozwa na Diamond Platnumz.

Dkt. Abbasi alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa waliokuja kushiriki kwenye hafla hiyo tarehe 14 Februari 2022 ambayo ni siku ya wapendanao (Valentine) na ghafla mshereheshaji wa hafla hiyo Zembwela kutangaza kuwa wasafi wameandaa keki maalum kwa Dkt Abbasi. 

Kwa upande wake Dkt. Abbasi aliishukuru Wasafi kwa kitendo hicho cha kumpa keki na kumwimbia wimbo wa kuzaliwa.

" Ndugu zangu niseme wazi kuwa sikutegemea wala kuwaza hii surprise, ninawashukuru sana, kitendo mlichonifanyia hakiwezi kunitoka kwenye kumbukumbu za maisha yangu." Alisisitiza Dkt. Abbasi.

Katika hafla hiyo wasanii mbalimbali walitumbuiza huku msanii maalum wa siku Zuchu akikonga nyoyo za washabiki huku mamake bi Hadija Kopa na Bosi wake Diamond Platinum wakiimba pamoja kwenye baadhi ya nyimbo na kushangiliwa na umati wa washabiki.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wanasiasa na watu mashuhuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com