Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MCHENGERWA-JIUPUSHENI NA RUSHWA, UVIVU NA UPENDELEO KWENYE SANAA TUWEZE KUFIKA MBALI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akikabidhiwa zawadi ya picha na Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) Dkt.Herbert Makoye mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo tarehe 09/02/2022 Wilayani Bagamoyo. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Watumishi wa Chuo cha Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo tarehe 09/02/2022 Wilayani Bagamoyo.Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Chuo cha Tamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) leo tarehe 09/02/2022 Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TasuBa) akiongozana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Mhe.Said Yakub na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Abdallah. Mkuu wa Taasisi ya TaSuBa Dkt.Herbert Makoye akimkaribisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa mara baada ya kuwasili Chuoni hapo leo tarehe 09/02/2022 wilayani Bagamoyo. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Chuo cha Tamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) leo tarehe 09/02/2022 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Abdallah akizungumza mara baada ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa kutembelea Chuo cha Tamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) leo tarehe 09/02/2022

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akikitazam kinanda kilichopo studio za TaSuBa mara baada ya kutembelea Chuo cha Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa)leo tarehe 09/02/2022 Wilayani Bagamoyo.Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Said Yakub na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah, wakiongozwa na Mkuu wa Taasisi ya TaSuBa Dkt.Herbert Makoye kwenye wakiangalia vifaa vilivyopo studio ya TaSuBa mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo tarehe 09/02/2022 Wilayani bagamoyo. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Tamaduni naa Sanaa Baagamoyo (TaSuBa) kuhusu uwepo wa Studio na ufanyaji kazi katika Chuo hicho mara baada ya kutembeleao Chuo hicho leo Wilayani Bagamoyo.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa, amezitakaa taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo hasa Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) kujiepusha na masula ya Rushwa, Uvivu, ubadhirifu na upendeleo kwenye tasnia ya sanaa ili kuweza kukuza sanaa nchini na itambulike kimataifa.

Ameyasema hayo leo mara baada ya kutembelea Chuo cha Tamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) kuona mikakati inayoendelea kufanyika katika Chuo hicho na kukitaja kuwa cha kimkakati kwa Taifa.

Aidha Waziri Mchengerwa ameahidi mageuzi makubwa ya chuo hicho na kukipa jukumu la kushirikiana na wadau kufanya utafiti wa falsafa ya muziki wa Tanzania (Tanzanian sound/beat).

Mchengerwa amesema kulingana na kauli ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu kuhusu kutafuta vijana wenye vipaji katika sanaa mtaa kwa mtaa, anategemea TaSuBa kusaidia kuwabaini vijana wenye vipaji na kuwasaidia.

Amesema Wizara inajipanga kuhakikisha Chuo hicho kinakuwa na Televisheni yake ambayo kukiwa na matamasha ya Utamaduni na Sanaa au matangazo mbalimbali yanayohusu sanaa yawe yanarushwa moja kwa moja kwenye televisheni hiyo.

Hata hivyo amesema suala la Rushwa, uzembe na upendelea ataendelea kupiga vita kwa maana yanashusha thamani na kuturudisha nyuma kama taifa, kila jambo linawezekana tunaweza tukashiriki mashindano makubwa ya kimataifa kama tutahamua.

Pamoja na hayo Mchengerwa amesema wapo katika mkakati wa kunazisha shule za michezo nchini ambazo zitakuwa daraja la kuinua vipaji vya michezo kwa vijana wa kitanzania mbao wapo mtaani.

"Tumekubaliana na watendaji kwamba tunakwenda kuanzisha shule 56 za michezo nchini ambapo shule moja itakuwa hapa Bagamoyo kwasababu ya mazingira lakini tutajipanga namna ya kufanya kuweza kuboresha baadhi yya viwanja vyetu ikiwemo kiwanja cha Mwanakalengwe kilichopo wilayani Bagamoyo". Amesema

Katika ziara hiyo Waziri Mchengerwa aliyeambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Mhe.Said Yakub Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Abdallah.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com