WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk.Damas Ndumbaro,akitoa uamuzi kwa waandishi wa habari kuhusu dosari zilizojitokeza katika mnada wa sita wa ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii baina ya Makampuni manne ya uwindaji wa kitalii na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) leo Februari 16,2022 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi,akizungumza wakati wa kikao kazi chenye kutoa maamuzi kuhusu dosari zilizojitokeza katika mnada wa sita wa ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii baina ya Makampuni manne ya uwindaji wa kitalii na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) leo Februari 16,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk.Damas Ndumbaro,akimkabidhi cheti cha ushindi Mwakilishi wa Trail Chasers Tanzania Ltd ambao wameshinda mnada wa vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya ki electroniki leo Februari 16,2022 jijini Dodoma.
....................................................
Na.Alex Sonna,DODOMA
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk.Damas Ndumbaro ametoa uamuzi wa kurudiwa kwa mnada kwenye baadhi ya vitalu vya uwindaji kitalii vilivyobainika kuwa na dosari katika mnada wa sita wa ugawaji vitalu uliofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA).
Hayo ameyasema leo Februari 16,2022 jijini Dodoma wakat akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Dk.Ndumbaro amesema kulijitokeza dosari kwenye mnada huo kwenye kampuni nne za uwindaji.
Amesema katika kampuni ya Bushman Hunting Safari LTD na TAWA ,baada ya kupitia hoja mbalimbali ameamua TAWA kuweka kwenye mnada mara moja kitalu Burko OA kwa kuwa kampuni hiyo iliyoweka dau la Dola za Marekani 400,000 kuomba kujitoa.
Aidha, amesema katika shauri la Kampuni ya Kilombero North Safaris LTD imeshindwa kuthibitisha malalamiko yake kwa kiwango cha mizania ya ulinganifu.
“Mwombaji(Kilombero) analalamika matokeo ya Kitalu cha Lake Natron GCA S kuwa Brenda Lyamuya aliyeshiriki mnada kwa niaba ya kampuni ya Robin Hurt Safaris Ltd, hakunja kampuni iliyosajiliwa Brela kwa jina lake, tumepitia hoja na kubaini malalamiko yake hayana msingi wowote kisheria,”amesema.
Dk.Ndumbaro amesema shauri la tatu lilikuwa kati ya Kampuni ya Tanzania Safari and Hunting (2003), TAWA na kampuni ya Trail Chassers Ltd katika mnada wa kitalu cha Selous GR MA 1 ambapo amesisitiza matokeo yam nada yatabaki yalivyo ambayo kampuni ya Trail ilishinda.
“Shauri jingine ni kati ya kampuni ya Trophy Belt Tanzania na TAWA ambapo ambapo imebainika kwamba shughuli za uwindaji wa kitalii sio miongoni mwa malengo ya Trophy Belt Tanzania Ltd hivyo kampuni hiyo haina uhalali na haiwezi kujihusisha na shughuli za biashara ya uwindaji wa kitalii,”amesema.
Amebainisha kuwa uamuzi aliotoa ni vitalu vyote vinne ambavyo kampuni hiyo ilishinda virudishwe kwenye mnada mara moia.