****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mara baada ya kufanikiwa kuichapa Kagera Sugar mabao 3-0 wenye dimba la Benjamini mkapa Jijini Dar es Salaam.
Fiston Mayele amekuwa akizidi kuwa bora kila kukicha mara baada ya leo kufanikiwa kupachika mabao mawili kwenye mchezo wa leo na kufikisha mabao tisa kwenye ligi ya NBC.
Mayele alianza kupata bao la maepma zaidi na kuisaidia timu yake iongozi mapema tu kabla ya baadae kupachika bao la pili akipokea pasi kutoka kwa Said Ntibazokiza.
Saidi Ntibazokiza nae hakuwa nyuma kwenye mchezo wa leo ambapo ametengeneza mabao mawili na lingine akipachika mwenyewe.
Social Plugin