*********************
EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua inayofuata kwenye michuano ya Azam Sport Federation Cup (ASFC) baada ya kuichapa timu ya Biashara United kwa mabao 2-1 kwenye dimba la Benjamini Mkapa.
Yanga Sc ilianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa beki raia wa DR Congo Yannick Bangala kwa bao zuri lililopeleka shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo mnamo dakika ya 22 ya mchezo.
Bao la pili la Yanga Sc lilipatikana kwa dakika ya 28 ya mcheezo kwa mshambuliaji wao Fiston Mayele kabla ya Biashara United kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Opare dakika ya 38 kipindi cha kwanza.
Social Plugin