Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZAMARADI AZUA GUMZO KUTUNDIKA BANGO BARABARANI KUMTAKIA VALENTINE NJEMA MUME WAKE

Zikiwa zimebaki saa chache tu kuingia Valentine’s day February 14 2022 Mtangazaji/Mjasiriamali @ZamaradiMketema ameingia kwenye trend mitandaoni baada ya kutundika barabarani bango lenye picha ya Mume wake likiwa na maneno ‘acha dunia ijue nakupenda kiasi gani, YOU ARE MY KING, happy Valentine’s day my love…… from your loving Wife”

Baada ya kusambaa kwa picha hii @ayotv_ ilimpigia simu Zamaradi ili kufahamu mengine ambapo amesema bango hili ambalo alianza kuliandaa kwa wiki mbili zilizopita bila Mume wake kufahamu, limewekwa leo February 13,2022 saa kumi na mbili jioni na amelilipia litakaa hapo kwa muda wa mwezi mzima "Hii ni barabara ambayo anapenda sana kupita yaani kila siku lazima apite ndiyo maana nimeliweka pale"

"Baada ya kuliweka nilimchukua mpaka pale amefurahi sana, tulipofika pale alicheka sana halafu akaingia kwenye gari machozi yakawa yanamtoka akaanza kulia akawa ameinama kwenye gari akasema kwa hiyo Mke wangu umeamua kuniweka hapa juu…… amefurahi sana kwa kweli”

“Sasa hivi tuna miaka mitano ya ndoa lakini sita ya mahusiano, nia yangu kumuweka kwenye bango ni jinsi ninavyompenda, ninampenda sana Mume wangu, Mume wangu amekuwa ni Mtu flani ambaye amenifanyia vitu vingi hakuna Mtu ambaye anaweza akajua” amesema Zamaradi.

“He is a special man in mylife nafikiri siku moja naweza kukupa Interview ambayo sijawahi kuitoa popote.... amekua ni Mtu ambae ananipenda sana hata maneno hayawezi kutosha kumuelezea ni Mwanaume wa namna gani kwenye maisha yangu", amemalizia Zamaradi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com