Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina Alvera Uwitonze mwenye ulemavu wa miguu, amefunguka na kusema amechoka kuwa single kwani sasa anaona ni kama anazeeka bila kuwa na mume.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 56, alisema kuwa hajawahi kuwa katika uhusiano wa mapenzi na mwanaume yeyote hapo awali na sasa anatafuta mtu wa kumuoa.
Katika mahojiano na Afrimax English, alisema anajuta kutowapa wanaume nafasi ya kuwa naye walipomkaribia wakati akiwa msichana mdogo.
“Walikuwa wakija hapa na kuniuliza wanioe nikawakatalia wote, niliogopa atakuja mwanaume kunipa ujauzito wakaniacha mimi na mtoto na kuendea mtu mwingine,” alisema Alvera.
Alvera aliendelea kueleza kwamba alipata mwanaume ambaye alikubali kumuoa lakini kwa masharti kwamba amlipe Ksh 22,000 (yaani mwanamke alipe pesa ambazo ni sawa na Tsh 446,000).
“Ninaishi kijijini ndanindani kabisa na hakuna njia ya kupata pesa za aina hiyo. Lakini nikipata, bado nitampa kwa sababu niko mpweke na pia nataka kuwa na familia yangu,” alisema.
Alvera, aliyezaliwa akiwa mzima wa afya bila ulemavu, alisema baada ya kuugua, wazazi wake walimpeleka kwa mganga badala ya hospitali hali iliyosababisha ugonjwa wake aliokuwa nao kuzaa ukilema.
Kwa sasa anaishi pekee yake huku akitegemea shughuli za kilimo shamba ili ajipatie kipato, anajipikia na ana redio ya zamani ambayo inamsaidia kutoa upweke.
Ameeleza kuwa, wanaume wengi wanasema kuwa muda wa kumuoa umepita na wanapendelea wanawake wabichi na ambao hawana ulemavu.
Social Plugin