Wadau wa mradi wa Tanzania ya kidigitali wakiwa kwenye kikao cha pamoja leo Jijini Dodoma kuzungumzia namna mradi huo utakavyowezesha kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja.
Katibu mkuu,Ofisi ya Rais, utumishi na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea leo Jijini Dodoma kwenye kikao kazi cha wadau wa masuala ya kidigitali.
**
Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 Blog-DODOMA.
SERIKALI kupitia Wizara ya habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora inatekeleza mradi wa Tanzania ya kidigitali (DTP) kwa lengo la kukuza uchumi wa kidigitali nchini.
Aidha mradi huo unatekekezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi 2026 huku gharama za utekelezaji zikiwa ni dola za marekani milioni 150 utakao boresha na kukuza ubunifu kwenye Tehama ikiwa ni pamoja na kuimarisha na kukuza biashara mtandao.
Hayo yameelezwa leo Jijini hapa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora, Dkt. Laurean Ndumbaro kwenye kikao cha kuanzisha mradi wa ujumuishwaji wa anuai za jamii kupitia mradi wa Tanzania ya kidigitali.
Amesema,mradi huo umegawanywa kwenye maeneo makuu matatu ikiwemo ikolojia ya kidigitali,uunganishaji wa kidigitali na jukwaa la huduma za kidigitali.
Dkt.Ndumbaro amefafanua kuwa ikolijia ya kidigitali itasaidia kujenga taifa la kidigitali kwa kustawisha mazingira wezeshi katika nyanja za uwekezaji kwenye Tehama na kuhakikisha faida za kidigitali zinawafikia wananchi ili kupata huduma bora kwa wakati.
"Sehemu hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha sera ,sheria kanuni na taratibu wezeshi kwa ajili ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa pamoja na kuboresha sekta ya mawasiliano nchini hali itakayo jenga uwezo wa Taasisi na vijana,wajasiriamali na biashara ndogo ndogo za kielektroniki,"amesema.
Akiwasilisha kuhusu utekelezaji wa mradi huo,Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Prisca Olomi ameeleza kuwa mradi huo utaboresha na kukuza maunganisho ya ndani na ya kimatifa ili kufikisha huduma za mawasiliano pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali za Serikali kwa wananchi.
Ameeleza pia matokeo ya mradi huo kuwa ni watumiaji milioni 13 kufukuzwa na huduma za mawasiliano na kuimarisha utoaji wa huduma za Serikali na miamala ya kielekroniki kwa wananchi.
Pamoja na hayo ameeleza kuwautasaidia kupatikana kwa intaneti kwa bei nafuu kitaifa ,kikanda na kimataifa ikiwa ni pamoja na kuongeza weledi kwa wataalamu wa Tehama ,vijana , wajasiriamali na Serikali.
Kwa upande wake mshiriki wa kikao hicho Mchungaji Petro Mpolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma amesema katika maendeleo ya kidigitali Wazee hawapaswi kuwa nyuma ili waende na wakati kupitia masuala ya Teknolojia na mawasiliano.
Amesema kupitia ushirikiswaji wa mabaraza ya Wazee yatasaidia kupelekea Tanzania ya kidigitali kimataifa zaidi na hatimaye kuwa na mchango kwenye uchumi wa viwanda.
Naye Mwenyekiti wa machinga Mkoa wa Dodoma Bruno Mponzi amesema"mradi huu ni fursa kubwa kwetu , tunaenda kunufaika na huduma ya kidigitali kwani huu mradi utarahisisha kufanya biashara,tutafanya biashara kidigitali na kuondokana na changamoto ya kuhama sehemu moja kwenda nyingine.
Tutatumia mfumo huu wa Tanzania kidigitali kupunguza adha tunazopata katika biashsara kwa kuwa mawasiliano yatarahisishwa kwa kuwa tunaondoka kwenye mfumo wa 3G kwendà 4G ambao utakuwa ba kaasi zaidi,"amesisitiza.
Social Plugin