KCU YAJIPANGA, WAKULIMA KUONGEZEWA BEI YA KAHAWA

 


Mwenyekiti wa KCU Ressy Mashurano (aliyevaa suti) akizungumza ,katikati ni
Makamu Mwenyekiti wa KCU Respicius John

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kagera KCU (1990) Ltd kimeongeza bei ya kahawa kwa mkulima kutoka shilingi 1,200 hadi shilingi 1,400 kwa kahawa ya kawaida na shilingi 3,000 hadi 3,300 kwa kahawa hai katika kipindi cha mwaka 2021/2022.

Akizungumza katika kikao cha waandishi wa habari na uongozi wa chama hicho, mwenyekiti wa KCU Ressy Mashurano amesema kuwa kwa kahawa ya kawaida wakulima wameongezewa shilingi 200 kwa kilo moja na kwa kahawa hai imeongezeka  shilingi 300.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa KCU (1990) Ltd Respicius John amesema kuwa mbali na kuongeza bei ya kahawa kwa wakulima, pia upo mfuko maalumu utakaowezesha wakulima kukopa kwa wakati ambao sio wa msimu wa kahawa, ili kuwaondolea tatizo la kuuza kahawa yao changa ikiwa bado shambani maarufu kama "Obutura".

John amesema kuwa chini ya utaratibu huo unaotarajiwa kuanza katika mwaka 2022/2023, wakulima watakopeshwa na KCU na watarejesha mkopo huo watakapovuna na kuuza kahawa yao. 

Sambamba na hayo ameongeza kuwa upo mpango wa kuanzisha Coffee Bar ambayo itakuwa sehemu maalumu ya kunywa kahawa bora na yenye viwango, ambayo itakuwa kielelezo cha kahawa inayozalishwa mkoani Kagera.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post