Waumini wapatao 30 wa Kanisa la Baptist lililopo kjiji cha Kakola kata ya Minkoto Wilaya ya Chato Mkoani Geita wamenusurika kifo baada ya jengo la Kanisa walilokuwa wanasali kuangushwa na upepo mkali ulioambatana na mvua na kuwafunika na kujeruhi watu 17.
Tukio hilo limetokea Machi 6 ,2022 majira ya saa 9 mchana ambalo tukio hilo licha ya kuangushwa Kanisa hilo, pia zaidi ya Nyumba 150 yakiwemo na Makanisa mawili zimeanguka kufuatia Mvua kubwa iliyoambatana na Upepo katika maeneo mbali ya Wilaya hiyo.
Mchungaji wa Kanisa la Baptist Minkoto Wilayni Chato Nicholas Vitus amesema Kanisa hilo liliangushwa na upepo na kuwa waumini 17 walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na kukimbizwa Hospitali kwa matibabu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Bathromew Manunga pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Philip Shoni wamefika eneo la tukio na kuthibitisha kuwa kaya zaidi ya 150 katika Wilaya hiyo zimeezuliwa na upepo mkali na mvua siku hiyo hiyo.
CHANZO - Mwangaza TV
Social Plugin