Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro inamshikilia mpiga debe wa Kituo cha Mabasi Msamvu,Abdallah Yassin (32) kwa tuhuma za kumchoma Kisu kifuani upande wa kushoto mpiga debe mwezake aliyetambuliwa kwa Jina la Tazani Mndeme (35) kutokana na ugomvi uliozuka baina yao kugombea Abiria na kusababisha kifo chake.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Fortunatus Muslimu amesema kuwa tukio hilo limetokea Machi 28,2022 majira ya Saa 12 asubuhi katika Stendi kuu ya mabasi Msamvu.
Muslimu amesema ugomvi huo ulisababisha mpiga debe Abdallah mkazi wa Mwembesongo,Manispaa ya Morogoro kumchoma kisu kifuani upande wa kushoto mwezake Tazani mkazi wa Kihonda ambaye alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro bahati mbaya alifariki Dunia wakati akipatiwa matibabu.
“Tayari mtuhumiwa Abdallah amekamtwa na hatua za kumfikisha mahakamani zitafuata mara upelelezi ukikamilika na Mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro” - Kamanda Musilimu.
Chanzo - Site Digital Media
Social Plugin