DC TARIME ASISITIZA WAZAZI KUWAPELEKA KLINIKI WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO


Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mntenjele

 Na Frankius Cleophace Tarime.

Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mntenjele amewahimiza wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF kuwapeleka kliniki watoto ambao wako chini ya miaka mitano ili waendelee kuwa na Afya njema.

Mkuu wa wilaya amebainisha hayo alipotembelea kaya  zinazonufaika na TASAF katika Halmashauri ya wilaya ya Tarime Vijijini na Mjini ili kuona jinsi gani wamenufaika na fedha hizo.

 Michael aliongeza kuwa kuna haja kubwa ya kupeleka watoto wadogo kliniki ili wawe na afya bora ili kipata wanachopata wanufaika wa mpango huo kisiende kwenye matibabu ya watoto kwa sababu ya kukosa huduma muhimu za awali zikiwemo chanjo.

“Tunajua fedha zinazotolewa ni kidogo sana lakini sasa tukizingatia kanuni za afya kwa kuwapeleka watoto kliniki nakupatiwa huduma itaondoa magonjwa nyemelezi ambapo mungetumia fedha hizo ili kuwatibu watoto hao sasa tumieni vyema fursa hiyo”, alisema Mkuu wa Wilaya.

 Licha ya Mkuu wa wilaya kusisitiza suala la kupeleka watoto kliniki amehimiza wazazi na walezi wakiwemo wale wanaonufaika na mpango wa TASAF kuwapeleka watoto shule hususani darasa la awali ili kuwajengea misingi bora wakiwa wadogo.

Mratibu wa kunusuru kaya Maskini TASAF Halmashauri ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara,  Emmanuel Kadama alisema kuwa fedha ambazo zimekuwa zikitolewa zimeweza kuwasaidia wanufaika hao kwa kuwapeleka watoto shule nakuwanunulia sare ambapo baadhi yao huwasaidia pia kwenye matibabu.

 “Kipindi mradi huu unaanza kuna kaya zilikuwa hazina uwezo wa kupata chakula kwa siku mara mbili lakini baada ya mpango huo sasa chakula, Mavazi na mahitaji ya family siyo shida nasisitiza kuendeleza miradi waliyonayo ili iwanufaishe”, alisema Emmanul.

Mmoja ya wanufaika wa mpango huo kutoka kijiji cha Borega,Royce Chacha  alisema kuwa kutokana na fedha anazozipata ameweza kununua kuku kwa ajili ya kufuga ambapo kuku hizo huuza mayai nakununulia watoto wake  vifaa vya shule ili waendelee na masomo.

 “Awali watoto wangu wa darasa la kwanza na la pili walishindwa kwenda shule kwa sababu ya kukosa vifaa lakini baada ya kupata hizi fedha za TASAF nafuga kuku nauza mayai nanunua vifaa vya shule”, alisema Royce.

Royce aliongeza kuwa kupitia mayai hayo yamekuwa yakiwasaidia watoto wake kuwapatia lishe bora.

Watoto takribani Milioni 2.6 chini ya miaka mitano hapa Tanzania wanatajwa kudumaa kutokana na lishe duni jambo ambalo linatajwa kuwa changamoto na hili kutatua changamoto hiyo serikali ilizindua rasmi Programu Jumuishi  ya Taifa ya malezi na makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (MMAM) ambapo programu hiyo itakuwa chachu ya maendeleo kwa makuzi ya awali ya mtoto.


 Kwani mtoto anapoanza kujengewa misingi bora akiwa tumboni usaidia kwa kiasi kikubwa kujenga ubongo wake hivyo kupitia mpango huo wenda ukawa mwarobaoni wa kusaidia changamoto zinazowakabili watoto kwa upande wa lishe bora.


 Akizindua Programu Jumuishi  ya Taifa ya malezi na makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (MMAM) Waziri wa Maendeleo ya jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum wakati huo ikiwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia wazee na watoto Dk: Doroth Gwajima aliaziagiza  Halmashauri zote nchini kuendelea na zoezi la ukusanyaji wa kiasi cha shilingi Elfu moja kwa ajili ya lishe shuleni ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa  program ya malezi na makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

Aidha  katika kutekeleza vyema mpango huo Naibu waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia masuala la walemavu Mh: Ummy Nderiananga  aliweka msisitizo kuwa Ofisi ya Waziri mkuu itashirikiana vyema na taasisi zoe katika kutekeleza vyema Programu Jumuishi  ya Taifa ya malezi na makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (MMAM).

 Pia malezi ya watoto chini ya miaka minane yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambapo husababisha watoto wengi kushindwa kukuwa ambapo asilimia 43 ya watoto wako kwenye hatari ya kutofikia  hatua timirifu ya ukuaji kutokana viashiria mbalimbali ikiwemo Utapiamulo.

 Katika mafunzo ya Waandishi wa Habari za Malezi, makuzi na maendeleo ya awali  ya Mtoto kutoka mikoa 26 Tanzania Bara  yaliyofanyika jijiji Dodoma Naibu Waziri  Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis katika ufungunzi wa mafunzo hayo aliopngeza kuwa  watoto zaidi ya Milioni 2.6  chini ya miaka mitano hapa nchini wamedumaa nakuomba waandishi wa habario kuendelea kuelimuisha jamii ili kuweza kutatua changamoto hiyo.

 Aliongeza kuwa zaidi ya watoto 270 waliochini ya miaka mitano hapa chini upoteza maisha kutokana na matatizo yanayotokana na Lishe duni nakusisitiza jamii kuzingatia suala la Lishe bora.

Mkurugenzi wa Shirika la Children In Crossfire (CiC)  Craig Ferla alisema kuwa  kuwa Programu ya mtoto kwanza  ambayo imezinduliwea itakuwa na malengo ya kuinua maendeleo ya watoto ili kuhakikisha kila mtoto anakuwa katika misingi bora.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post