Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking : HAYA HAPA MAJINA YA MAKATIBU WAPYA WA UVCCM WILAYA WALIOTEULIWA


Uteuzi huu unajumuisha sura mpya, waliobadilishwa vituo vya kazi


NA GODFREY NNKO

SEKRETARIETI ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa katika kikao chake kilichofanyika Machi 30,2022 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete (Convention) jijini Dodoma imefanya uteuzi wa Makatibu wa UVCCM wilaya na kufanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya makatibu wa UVCCM.


Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Bw.Kenani Kihongosi.


"Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi inapenda kuwajulisha wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi na wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwamba, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30/03/2022, Ukumbi wa Jakaya Kikwete (Convention) jijini Dodoma, kimefanya uteuzi wa makatibu wa UVCCM wilaya kama ifuatavyo;

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com