Mkurugenzi wa kampuni ya Heritage Microfinance na Kipong bar,Sia Kassian amepata Tuzo mbili kwa mpigo moja ikiwa ya Taasisi ya kifedha na yapili huduma ya chakula na vinywaji
Mkurugenzi wa Aika Classic,Aika Kessy amejinyakulia Tuzo ya mbunifu wa mitindo
Mkurugenzi wa mgahawa maarufu Kitamu Afrika,Leah Assenga alipata Tuzo ya mgahawa bora
Mkurugenzi wa kampuni ya African Wear & Design,Jenifer Alphayo alishida Tuzo ya ushonaji
Bi Eva Nyambura alipata Tuzo katika nyanja ya kikundi bora cha mazingira
**
Na Pamela Mollel,Arusha
Wanawake walioshinda Tuzo za Malkia wa Arusha waeleza chanzo cha ushindi wao kuwa ni Bidii, Kujituma na Nidhamu katika kazi ndiyo chanzo cha kuibuka Malkia wa Nguvu mkoani Arusha 2022.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana jijini Arusha mara baada ya kutunukiwa tuzo hizo washindi hao wamewashauri wanawake nchini kujituma na kuacha tabia ya utegemezi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Heritage Microfinance, Sia Kassian ambaye alijinyakulia tuzo mbili katika nyanja ya taasisi ya kifedha sanjari na huduma ya vinywaji alisema kwamba nidhamu,bidii na kujituma ndivyo vimemfanya afike mahali alipofika.
Mkurugenzi wa kampuni ya ViolaTours,Violet Mfuko ambaye alinyakua tuzo katika nyanja ya utalii aliwataka wanawake kujituma na kuacha tabia ya kulalamika mara kwa Mara.
"Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuonyesha njia sisi wanawake lakini wanawake tufanye kazi sasa tuache kulalamika", alisema Mfuko.
Hatahivyo,mfanyabishara Aika Kessy ambaye ni mmiliki wa duka la Aika Classic aliyejinyakulia tuzo katika nyanja ya ubunifu na mitindo alisema kwamba tuzo hiyo imempa hamasa katika kufanya kazi kwa juhudi na bidii tofauti na hapo awali.
Mshindi katika tuzo ya mgahawa bora Leah Assenga mmiliki wa mgahawa wa Kitamu Afrika alisema kwamba tuzo aliyoipata ni mwendelezo wa tuzo nne alizopata ambapo tuzo mbili alizipata kimataifa na zimezidi kumpa hamasa ya kufanya vizuri zaidi.
"Nimefurahi kushinda hii tuzo hii inakuwa ya nne sasa maana tuzo mbili nilishinda kimataifa na mojawapo ni Traveller's Choice Award hakika mgahawa wetu wa Kitamu umeniletea heshima ndani na nje kimataifa", alisema Assenga
Eva Nyambura aliyenyakua tuzo katika nyanja ya kikundi bora cha mazingira aliwataka wanawake nchini kutambua kuwa hakuna siri ya ushindi katika maisha yao zaidi ya kujituma katika kazi na bidii.
Mmiliki wa kampuni ya African Wear & Design Jeniffer Alphayo ambaye alijinyakulia tuzo katika nyanja ya ushonaji aliwashukuru waandaji wa tuzo hizo kwa kuwa zinawapa hamasa katika kufanya kazi zao na zinatambua mchango wao katika jamii.
Mwandaaji wa tuzo hizo,Phide Mwakitalima ameomba serikali kuwaunganisha wanawake hususani wajasiriamali hapa nchini ili waweze kufanikiwa katika shughuli zao