Sophia Jongo Kamanda wa Polisi Tanga |
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga, Safia Jongo ameeleza kuwa mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Machi 28, 2022 baada ya Mohammed kumkuta mkewe Rehema Barau akiwa na Athumani ndani nyumba yao ambapo alianza kumshambulia.
Kamanda Jongo amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya mtuhumiwa wa mauaji Mohammedi kumshambulia Athumani hadi kufa.
Ameongeza kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kujua undani wake, muhusika aliyefanya tukio hilo ameshakamatwa.
"jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na tutatoa taarifa zaidi," amesema Kamanda Jongo.
"jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na tutatoa taarifa zaidi," amesema Kamanda Jongo.
Social Plugin