Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHANGAMOTO YA UPOTEVU WA MAZAO YA WAKULIMA WAKATI WA MAVUNO YAPATIWA UFUMBUZI


Mkurugenzi wa kampuni ya Imara Teknolojia ya jijini Arusha, Alfred Chengula akielezea mashine ambazo wameweza kuzibuni ikiwemo ya kupukuchua na kupura mazao ya aina Tisa .

Na Rose Jackson,Arusha.

Upotevu wa mazao ya wakulima wakati wa mavuno unaowakabili wakulima wengi sasa umepata ufumbuzi baada ya baadhi ya watafiti kugundua mashine yenye uwezo kudhibiti tatizo hilo.

Akielezea mafanikio hayo jijini Arusha kwa waandishi wa habari waliotembelea kampuni ya Imara Teknolojia ya jijini Arusha kwa lengo la kujifunza habari kwa vitendo ,mara baada ya kupatiwa mafunzo na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mtafiti na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alfred Chengula amesema mashine hiyo ina uwezo wa kuwasaidia wakulima kupukuchua mazao ya aina mbalimbali yakiwemo mahindi.

Amesema wameweza kubuni mashine mbili tofauti ambapo mojawapo inapukuchua na kupura mazao tisa tofauti Kama mahindi, Alizeti, maharage mbaazi,choroko na mengineo , ambapo walibuni ili iwasaidie wakulima wadogo na wajasirimali.

Mashine hii inatumia boda boda na ina uwezo wa kupukuchua mahindi gunia mia mbili kwa siku moja tofauti na awali ambapo wakulima walikuwa wanatumia muda mrefu kupiga piga mahindi.

Ametaja mashine ya aina ya pili ambayo wameweza kubuni ni ya kuchakata na kubaraza nafaka mbalimbali kwa ajili ya chakula cha mifugo.

Amedai kuwa mashine hii ina uwezo wa kusaga magunzi ,kukata majani kama mabua na ina uwezo wa kubaraza mahindi na mashudu kwa ajili ya kulishia mifugo.

"Mashine hizi tunazitengeneza wenyewe na lengo letu ni kuwasaidia Wakulima na Wafugaji waweze kufikia malengo yao kwa muda mdupi zaidi kwa kuboresha maisha yao",aliongeza.

Chengula amesema kuwa pamoja na kupata mafanikio hayo ya kubuni mashine hizo lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya kuboresha miundo mbinu yao ya kazi hivyo anaamini mara baada ya COSTECH kutembelea kampuni hiyo itamwezesha kutatua changamoto hiyo illi kuweza kufikia ndoto za utengenezaji wa mashine ambazo wameshazifanyia tafiti.

Baadhi ya wakulima waliofikiwa na teknolojia hizo ameeleza kuwa mashine hiyo imemsaidia kupukuchua mahindi kwa muda mchache iikiwa ni pamoja na kueleza changamoto zake ikiwemo ya uwezo mdogo wa kumudu gharama .

Licha ya watafiti kufikia mafanikio hayo na faida zilizoanza kupatikana ,ili lengo liweze kutimia ushirikishaji wa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia COSTECH na pia taasisi za fedha unahitajika .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com