Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Jeniviva Timotheo (29) mkazi wa Tarafa ya Inyonga Mkoani Katavi ameuwawa kwa kuchinjwa na mume wake aitwaye Anisent John (32) na kisha mwanaume huyo kujinyonga kwa kutumia chandarua baada ya kutekeleza mauaji hayo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad amesema tukio hilo limetokea mnamo Machi 2,2022 katika Kijiji Cha Mtakuja Kata ya Nsenkwa Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi ambapo mara baada ya kutekeleza mauwaji hayo mume wa marehemu Bw.Anisent John nae alijinyonga kwa kutumia chandarua na kisha kuacha ujumbe kuwa amejiua kwa hiari yake mwenyewe.
"Mtuhumiwa ambaye ni marehemu, siku ya tukio alifunga mlango wa chumba chao kisha kumuua Mke wake,ambapo mara baada ya kutekeleza mauaji hayo nae alijinyonga kwa kutumia chandarua aliyoining'iniza kwenye kenchi ya dari chumbani kwake",Alisema ACP Hamad.
ACP Hamad amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia unaohusishwa na wivu wa kimapenzi na miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi kisha kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Hata hivyo ACP Hamad amesema kuwa hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusishwa na tukio Hilo.
Chanzo - Site Tv
Social Plugin