Bernard Membe akiwa kwenye moja ya kazi za CCM
*
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Taifa kilichofanyika leo Machi 31, 2022 Jijini Dodoma, kimeamua kumrejeshea kadi mwanachama wake Bernard Membe ambaye alifutiwa uanachama.
Membe pamoja na wanachama wengine waliorejeshewa kadi zao watakabidhiwa kwenye maeneo waliyopo.
Membe ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwenye serikali ya awamu ya nne, alifukuzwa uanachama wa CCM Februari 28, 2020 kufuatia uamuzi ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Taifa.
Social Plugin