Yusufu Juma Mwenda
**
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi amemteua Yusufu Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Zenna Saidi, uteuzi wa Mwenda umeanza rasmi Machi Mosi.
Kabla ya uteuzi huo, Mwenda alikuwa Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Jijini Dar es Salaam alipofanya kazi kwa miaka kadhaa hadi alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
Aidha Mwenda aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Msasani na Meya wa Manispaa ya Kinondoni katika Serikali ya awamu ya awamu ya nne iliyokuwa chini ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Social Plugin