Mnamo Jumanne, Machi 01, 2022 Katika mahakama ya Kibera, Zainab alishitakiwa kwa kosa la kumsababishia jeraha mwanaume aliyejulikana kama, Joseph Karanja, baada ya kumpa KSh 100 (takribani shilingi 2000 za Tanzania) kama nauli ya kurudi nyumbani.
Inadaiwa kuwa Zanab alimuingiza kwenye maumivu mwanaume huyo waliokuwa kwenye baa wakinywa vinywaji muda wa saa nane usiku Februari 21, 2022 huko Kangemi, Nairobi.
Wawili hao walikuwa wametofautiana katika jaribio la kusuluhisha maswala ya uhusiano wao uliokua na migogoro binafsi ya kimapenzi.
Mwanaume huyo alimshutumu mwanamke wake kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine na ugomvi ukazuka huku wakiendelea kunywa pombe.
Baada ya kushindwa kukubaliana, Bi Ochero alimwomba Bw Karanja akodi usafiri wa kumpeleka nyumbani Kawangware lakini akampa Sh100 za Kenya ambazo kwa Tanzania ni sawa na shilingi 2000.
Bi Ochero aliambia polisi kuwa alisisitiza kwamba Karanja akodi mwendesha bodaboda ili ampeleke nyumbani lakini Karanja alidaiwa kuanza kumbishia, Pia aliwaambia polisi kwamba alikuwa amelewa kabisa na baada ya hapo anakumbuka tu alipoamka na kujikuta katika kituo cha polisi cha Kangemi baadaye siku hiyo hiyo.
Ripoti ya polisi ilieleza kuwa mwanamke huyo kwa hasira alimrukia mwathirika na kuchomoka na sikio lake la kushoto kabla halijaanguka chini.
Alipoona sikio lake likiwa chini, Karanja alilinyanyua na kulibeba kwa uangalifu kwenye begi la karatasi na kulipeleka hospitali kwa matibabu.
Mwanamme huyo aliambiwa atafute matibabu zaidi katika hospitali nyingine huko Eastland, ambako aliambiwa kuwa sikio lilikuwa limeharibika kabisa na alihitaji upasuaji wa plastiki baada ya matibabu ya miezi mitatu.
Mshukiwa alikanusha mashtaka mbele ya hakimu Charles Mwaniki. Aliachiliwa kwa dhamana lakini Kesi hiyo itatajwa tena Machi 16.
Social Plugin