Luwizo akiwa na wake zake
Mwanaume Mcongo aliyetambulika kwa jina Luwizo ndiye ameingia kwenye rekodi ya mfalme Solomoni hivi punde.
Luwizo, mwanaume mwenye wake wengi kutoka Kalehe, Kivu Kusini, DR Congo, hivi majuzi alioa mapacha watatu Natasha, Natalie, Nadege katika sherehe ya harusi ya kupendeza.
Katika mahojiano na AfriMax, Luwizo alifichua kwamba mwanzo Natalie ndiye alikuwa ameteka moyo wake baada yao kukutana kwenye mtandao wa kijamii.
Kila Luwizo alipokuwa akitembelea Natalie nyumbani kwake, na kumkosa, alikuwa akikaribishwa na mmoja wa pacha hao ambao alishindwa kuwatofautisha.
Siku zilipoendelea kusonga, pacha wote watatu walizinguliwa na penzi lake. Luwizo alisema alishtuka kupatana na wanawake watatu wanaofanana alipomtembelea Natalie akitaka waidhinishe ndoa yao. Lakini warembo hao walimwambia wanataka awaoe wote.
"Mwanzoni tulipomwambia kwamba anatakiwa kutuoa sote alishtuka, lakini kwa sababu tayari alikuwa ametupenda sote, hakuna kitu ambacho kiliweza kuzuia mipango yetu kwani pia tulikuwa tunampenda. watu wanaona kuwa haiwezekani kwa wanawake watatu kugawana mume mmoja, lakini kwetu, kugawana kila kitu imekuwa maisha yetu tangu utotoni,” Natalie, mmoja wa mapacha hao watatu alisema.
Akizungumzia tukio hilo Luwizo alisema: "Karibia nizimie. Nikawauliza kati yenu nyote, Natalie ni nani? Wakaniambia nimekutana nao siku tofauti tofauti nilizomtembelea. Nilichanganyikiwa kwani nilikuwa na mpango wa kuolewa na Natalie lakini kilichonichanganya ni kwamba singeweza kuoa mmoja wao na niwaache wale wawili." Aliongeza kuwa:
"Nililazimika kuwaoa wote kwa sababu ni mapacha watatu. Haukuwa uamuzi rahisi kwa sababu hadi sasa, wazazi wangu hawaelewi ninachofanya."
Luwizo alibadilishana viapo vya ndoa na pacha hao katika hafla ya faragha iliyohudhuriwa na marafiki wa karibu na familia ingawa wazazi wake hawakuhudhuria harusi hiyo
"Lazima upoteze kitu ili upate kingine. Isitoshe, mtu ana matakwa yake na namna yake ya kufanya mambo. Kwa hiyo nina furaha kuwaoa hao mapacha watatu bila kujali wengine wanafikiria nini. Wazazi wangu walidharau uamuzi wangu ndiyo maana waliniona. sikuhudhuria harusi yangu. Lakini ninachoweza kusema ni mapenzi hayana kikomo," alisema.
Akizungumzia ndoa yao, Natalie alisema: "Tuna furaha sana. Ndoto yetu ilitimia. Tulifikiri tungetenganishwa na ndoa, lakini Mungu alisikia maombi." Dada yake Luwizo alisema amefurahishwa naye na ataunga mkono uamuzi wake kila wakati. "Mwanzoni niliposikia anaoa mapacha watatu sikuelewa lakini baadaye nikaelewa inawezekana, ingawa wazazi wetu walimdharau, nitamuunga mkono kila wakati," alisema.