MWANAMKE KIONGOZI
1. Ninaanza
kwa Imani, kumshukuru Mwenyezi
Kwa rehema na amani,upendo tunauenzi
Turudishe shukrani, kwa yake mema
mapenzi
Mshikamano na Amani, tuendelee kuvienzi
2. Nampongeza
wa sita Rais kashikilia
Kamwe hakusitasita, uongozi shikilia
Miongoni mwa nchi sita, mwanamke kashikilia
Mshikamano na Amani, tuendelee kuvienzi
3. Kwa
yake kauli mbiu,kazi inaendelea
Usafiri,afya elimu,mapambano
yanaendelea
Umeme,maji ,nidhamu,yote
yanaendelea
Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi
4. Mwanamke
ni kama moyo,unaosukuma maendeleo
Bila ya upendeleo,yapo mengi
mafanikio
Amehaidi kwa kiapo,kuongoza kwa
mfano
Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi
5. Mengi
yanatukumbusha awamu ile ya tano
Mikono kuchangamsha,uvivu kusema no
Hii inahamasisha,mingine yetu mitano
Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi
6. Ushupavu
ujasiri,ndio chake kipaumbele
Kawaweka mstari, Wanawake kifua
mbele
Kusifika kwa mazuri, kwenye sekta zote za mbele
Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi
7. Wanawake
tunaweza kusukuma hii dunia
Siku yetu tumeweza ,kutangaza yetu
nia
Nyota tumeiangaza, bila ya kukata
nia
Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi
8. Kwa
pamoja twaahidi, kushirikiana nawe
Kwa bidii na juhudi, kusimama nawe
Nyuma kamwe haturudi,kupingana nawe
Mshikamano na Amani tundelee kuvienzi
9. Muda
nao si rafiki mmoja mwaka umepita
Ilani tumeiafiki,demokrasia imepita
Tena bila ya unafiki kwa Imani
utapita
Mshikamano na Amani tundelee
kuvienzi
10. Kalamu
naweka chini mama samia hongera
Tumuombee kwa Imani aliyetoka kwa
dharura
Ameilinda yake Imani,kuitekeleza
dhamira
Mshikamano na Amani tundelee
kuvienzi
Asante
Imeandaliwa na
mwanamke
0714496369
Women innovators 4 Women
Empowerment
Social Plugin