Na Mbuke Shilagi - Kagera
Wananchi wa Kata ya Bakoba Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wamekubali eneo lilipo soko la Nyakanyasi katika Kata hiyo kubadilishwa matumizi na kujengwa Kituo cha Afya.
Wamesema hayo katika mkutano wa Kata wa hadhara uliokuwa umelenga kutoa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa kata hiyo.
Wananchi wa Kata hiyo wamesema kuwa jambo hilo ni jema kutokana na soko hilo kuwa na wafanya biashara wachache huku wakiiomba serikali kuwatafutia wafanyabiashara hao eneo lingine.
Aidha katika mkutano huo Diwani wa Kata hiyo Mh. Shabani Rashid alipendekeza eneo la soko hilo kugeuzwa matumizi na badala yake kijengwe Kituo cha Afya kauli ambayo wananchi walifurahishwa nayo na kushangilia ishara ya kukubaliana na wazo hilo.
Huku akisema kuwa katika utekelezaji wa Ilani serikali inayo mpango wa kujenga Kituo cha Afya katika kata hiyo ili kuondoa adha kwa wananchi wanao kwenda vituo jirani.
Diwani wa Kata ya Bakoba Mh. Shabani Rashid akihutubia hadhara
Muonekano wa soko la nyakanyasi katika Kata ya Bakoba
Social Plugin