Tembo
Mfugaji aitwaye Narudwasha Titika, mkazi wa kijiji cha Alaitore kilichopo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, amefariki dunia jana Machi 9, 2022, majira ya saa 7:00 mchana baada ya kushambuliwa na Tembo sehemu mbalimbali za mwili wake, wakati akitafuta kuni.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo, na kusema kwamba uchunguzi wa awali wa jeshi hilo umebaini kuwa marehemu alikutwa na mkasa huo wakati akitafuta kuni akiwa na wenzake ndani ya hifadhi hiyo.
Social Plugin