Mkurugenzi Mkuu wa taasisi na usanifu wa mitambo Tanzania (TEMDO ) Mhandisi Fredrick Kahimba akiwa na mkurugenzi wa menejimenti ya maarifa kutoka COSTECH Dr. Philbert Luhunga pamoja na waandishi wa habari akielezea teknolojia zinazozalishwa katika taasisi hiyo Mara baada ya Waandishi kutembelea TEMDO kwa lengo la kujifunza habari za matokeo ya utafiti.
*****
Rose Jackson,Arusha.
Tume ya sayansi na teknolojia Tanzania COSTECH imetoa mafunzo ya siku nne kwa waandishi wa habari Mikoa ya Kanda yw Kaskazini na watafiti lengo likiwa ni kuhakikisha taarifa za utafiti na ubunifu zinaandikwa kwa lugha rahisi ambayo itawafanya wananchi kuelewa.
Akizungumza katika semina ya mafunzo hayo inayofanyika jijini Arusha mkurugenzi wa menejimenti ya maarifa kutoka COSTECH Dr Philbert Luhunga amesema kuwa kuna matokeo mengi ya utafiti ambayo wananchi Wanapaswa kuyaelewa kupitia waandishi.
Amesema kuwa waandishi wanapoandika habari za sayansi na matokeo ya utafiti wataweza kuibadilisha jamii na kuleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuwa wananchi watapata taarifa za utafiti ambazo zitaleta maendeleo endelevu.
"Tumekuwa na tafiti mbali mbali kutoka taasisi za utafiti na tumeona Kuna matokeo mengi ya utafiti ambayo wananchi Wanapaswa kufahamu hivyo tunaamini kuwa waandishi wanapaswa kuandika habari hizi ziwafikie wananchi kwa kuwa ndio walengwa wakubwa wa kujua matokeo ya tafiti hizo",alisema Dr. Luhunga.
Aidha Dr Luhunga amewasihi wanahabari kuhakikisha wanaisemea mazuri serikali kwa kuandika mema ,huku akiwataka waandishi kujiheshimu na kujitambua.
Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo Dr Sigsbert Mmasi kutoka taasisi ya usanifu wa mitambo Tanzania (Temdo) amesema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kubuni teknolojia mbali mbali ikiwemo mashine na vitendea kazi vya hospitalini ambavyo vimekuwa Ni mkombozi wa wananchi katika kurahisisha shughuli.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hao Noeli Urasa amesema kuwa anashukuru COSTECH kwa kutoa mafunzo hayo kwani yamempa uelewa wa kuandika habari za matokeo ya utafiti ambazo zitawezesha jamii kupata majawabu ya changamoto wanazokabiliana nazo.
Social Plugin