RAIS SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA AKIWEMO BALOZI HUMPHREY POLEPOLE


Rais Samia Suluhu Hassan, leo Machi 15, 2022 amewaapisha viongozi wawili aliowateua hapo jana, ambao ni Humphrey Polepole aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi na Waziri Kindamba aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao, imefanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.
Rais Samia akimuapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 15 Machi, 2022.

Kabla ya uteuzi huo, Polepole alikuwa Mbunge wa Kuteuliwa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kindamba alikuwa Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Rais Samia Suluhu Hassan akimuapisha Waziri Kindamba Waziri kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe .

“Mh. Balozi najua baada ya hapa watakuweka darasani kwanza pale Chuo cha Diplomasia, utakapotoka pale kabla hujaenda Malawi nitakutana na wewe, kwahiyo tutazungumza kwa urefu,”-Rais Samia
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba Waziri akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi Humphrey Polepole wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba Waziri na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post