Vidonge hivyo vitafanyiwa majaribio kwa wanaume mwishoni mwa mwaka huu.
**
Timu ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota ikiongozwa na Dr Abdullah Al Noman imegundua kidonge cha uzazi wa mpango kwa wanaume baada ya kufanya majaribio kwa panya na kufanikiwa kwa asilimia 99.
Tangu kidonge cha kuzuia mimba kwa wanawake kilipogunduliwa, wanasayansi waliendelea kufanya utafiti kwa upande wa wanaume ili watu wote wawe na jukumu sawa la uzazi wa mpango.
Kidonge hicho kitapunguza uwezo wa mwanaume kumpa mimba mwanamke kwa muda, na kitafanyiwa majaribio kwa wanaume mwishoni mwa mwaka huu.