Picha za setlaiti kutoka kwa kampuni ya teknolojia ya Maxar zinasema kwamba ripoti za mapema zinazosema kwamba msafara wa magari ya kijeshi ya Urusi una urefu wa kilomita 27 sio za kweli.
Ukweli ni kwamba msafara huo wa magari ya kijeshi una urefu wa kilomita 64, kulingana na Maxar.
Kampuni hiyo iliongezea kwamba , picha mpya ardhini zilikuwa zinaonesha wanajeshi walio ardhini na helikopta za kutekeleza mashambulizi kusini mwa Belarus, ikiwa ni chini ya maili 20 kutoka mpaka wa Ukraine.
Takriban wanajeshi 70 wameuawa katika shambulio la mizinga la Urusi, maafisa wa Ukraine wamethibitisha.
Wafanyakazi wa dharura wanajaribu kutafuta manusura katika Kituo cha kikanda cha Kherson ambacho sasa kimezingirwa na wanajeshi wa Urusi, zinasema ripoti, huku wanajeshi na vifaa vya kijeshi vimeripotiwa kuwepo "pande zote".
Jeshi la Urusi linaendelea kusonga mbele kwa kasi huko Kyiv, na picha za satelaiti zinazoonyesha msafara wa kivita ambao una urefu wa maili 40 (65km.
Makumi ya raia waliuawa mapema Jumatatu katika shambulio la makombora la Urusi kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kharkiv.
Serikali ya Ukraine imesema inapanga kuuza hati za kivita ili kulipia vikosi vyake vya kijeshi.
Takriban wanafunzi 460 wa Ghana wameondoka Ukraine wakielekea Poland, Hungary, Romania, Slovakia na Jamhuri ya Czech kufuatia uvamizi wa Urusi, Waziri wa Mambo ya Nje Shirley Ayorkor Botchwey amesema.
Wanafunzi hao watapokelewa na maafisa kutoka balozi za nchi hizo na maafisa wa vyama vya wanafunzi wa Ghana.
Wanatarajiwa kurejea Ghana katika siku zijazo.
Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wamealikwa na serikali katika mkutano katika mji mkuu wa, Accra, siku ya Jumanne.
Awali serikali ilikuwa imewataka wanafunzi wa Ghana nchini Ukraine kutafuta makazi katika nyumba zao au katika maeneo yaliyotengwa na serikali.
Zaidi ya raia 1,000 wa Ghana kwa sasa wanasoma au kufanya kazi nchini Ukraine.
Baadhi ya Waafrika walikuwa wamelalamikia ubaguzi wa rangi katika mpaka wa Ukraine na Poland.