Na Edwin Soko -Mwanza
Mashindano ya kupiga kasia kwa akina mama yamefanyika leo Jijini Mwanza ikiwa na kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wavuvi wadogo Duniani, mashindano hayo yameandaliwa na Wizara ya Uvuvi na Mifugo kwa kushirikiana na FAO pamoja na shirika la EMEDO.
Mgeni rasmi kwenye mashindano hayo Bi. Agnes Majinge alisema kuwa, ni furaha kuona mashindano hayo ya kupiga kasia kwenye Mitumbwi yakihusisha wanawake hiyo ni ishara tosha ya Mwanamke anaweza kufanya kazi kwenye kila sekta yoyote ile.
"Ni faraja kuona kwenye uvuvi mdogo wanawake wapo na wanafanya kazi za uvuvi na kuchangia uchumi wa Taifa kama wanavyofanya wanaumwe." alisema Bi Majinge.
"Shirika la EMEDO linatambua mchango wa wavuzi wadogo Duniani kwenye kuelekea maadhimisho ya kielele cha siku ya wavuvi Duniani kitakachofanyika kesho Machi 7, 2022", alisema Mkurugenzi wa shirika la EMEDO Editrudith Lukanga.
Mashindano hayo kupiga kasia yamefanyika ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya wavuvi wadogo Duniani yatakayofanyika kesho Jumatatu Machi 7, 2022 kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Wizara ya Uvuvi na Mifugo kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani FAO na Shirika la EMEDO ndio waandaaji wa maadhimisho hayo ya mwaka huu.
Mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza walishuhudia wanawake wakichuana kwenye kupiga kasia ili kujishindia zawadi ya fedha taslimu.
Hii ni muendelezo wa burudani kwa wakazi hao ambao baadaye watashuhudia mtanange wa kukata wa shoka wa ligi kuu ya NBC kati ya klabu ya Yanga na Geita Gold.