Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAWAKE NSSF WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MAHITAJI KWA WANAWAKE NA WATOTO WALIOLAZWA HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA

Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanawake wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga wamesherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mahitaji hayo leo Ijumaa Machi 11,2022 katika wodi za wanawake na watoto, Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi amesema wamefika katika hospitali hiyo ili kutoa faraja kwa wanawake na watoto ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya Wanawake Duniani ambayo husherehekewa ulimwenguni kote Machi 8.

“Sisi wanawake kutoka NSSF Shinyanga tumekuja hapa kusherehekea siku ya wanawake duniani na wanawake ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa kuleta mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni za unga na miche, mafuta ya kujipaka,pipi,biskuti, maji na juisi”,amesema Mdabi.

Naye Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo amewashukuru wanawake hao kwa kufika katika hospitalini hapo na kutoa mahitaji kwa akina mama na watoto waliolazwa.

Nao akina mama waliolazwa katika hospitali hiyo wamewashukuru wanawake hao kutoka NSSF mkoa wa Shinyanga kwa kuwapatia mahitaji hayo ambayo yatawasaidia katika kipindi hiki wakiendelea kupatiwa huduma za matibabu hospitalini hapo.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi akizungumza wakati Wanawake wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani leo Ijumaa Machi 11,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (wa nne kulia) akizungumza wakati Wanawake wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (kushoto) akizungumza wakati Wanawake wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Sehemu ya mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni za unga na miche, mafuta ya kujipaka,pipi,biskuti, maji na juisi vilivyotolewa na Wanawake wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akikabidhi sabuni ya unga na mahitaji mengine kwa Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (wa nne kulia) kwa ajili ya wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akikabidhi sabuni ya unga na mahitaji mengine kwa Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (wa nne kulia) kwa ajili ya kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani.
Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (katikati) akiangalia mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na Wanawake wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Wauguzi na wanawake wafanyakazi NSSF Shinyanga wakijiandaa kugawa mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani
Wauguzi na wanawake wafanyakazi NSSF Shinyanga wakijiandaa kugawa mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi akikabidhi mafuta ya kujipaka kwa mmoja wa wanawake wodini. Kila mwanamke wodini amepatiwa mafuta,sabuni ya unga na mche,juisi, pipi na maji.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi akikabidhi mafuta ya kujipaka kwa mmoja wa wanawake wodini. Kila mwanamke wodini amepatiwa mafuta,sabuni ya unga na mche,juisi, pipi na maji
Wanawake NSSF Mkoa wa Shinyanga wakimwangalia mtoto aliyelazwa wodini wakati wakikabidhi mahitaji mbalimbali.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akikabidhi sabuni  na mafuta kwa mmoja wa wanawake wodini
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akizungumza na mama anayeuguza mtoto wake wodini
Wanawake wafanyakazi NSSF Mkoa wa Shinyanga wakiwa wodini
Zoezi la kukabidhi mahitaji mbalimbali wodini likiendelea
Zoezi la kukabidhi mahitaji mbalimbali wodini likiendelea.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com