Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ARUSHA WOMEN IN BUSINESS WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI....DR. ATUKUZWE AHAMASISHA WATANZANIA KUCHANGIA DAMU

 Na Woinde Shizza , ARUSHA
Watanzania wametakiwa kujijengea tabia ya kuchangia damu mara kwa mara ili kuweza kupunguza tatizo hilo la upungufu wa damu salama katika benki  ya damu pamoja na kuwasaidia  watoto pamoja na watu wazima wenye tatizo la saratani  (Kansa)za aina mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na daktari kutoka kitengo cha magonjwa ya Kansa katika  hospitali  ya rufaa ya Kanda ya kaskazini (KCMC) Dr. Atukuzwe Kahakwa alipokuwa akiongea katika sherehe za  maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yaliyoandaliwa na kikundi cha Arusha Women in Business Saccos ltd  yaliyofanyika katika ukumbi wa Arusha Corridor Spring ambapo maathimisho hayo yalitanguliwa na maandamano  ya wanawake hao

Alisema kuwa katika kitengo saratani kuna uhitaji mkubwa sana wa damu kutokana na wagonjwa wengi wa Kansa kutakiwa damu nyingi ,kwani baadhi yao ugonjwa huo unasababisha kupunguza damu Kwa kasi kubwa

"Mfano pale kwetu KCMC katika kitengo Cha Saratani tumekuwa tunapokea watoto wengi wenye ugonjwa wasaratani ya damu hivyo unakuta kutokana na tatizo hilo damu yao inaisha mapema na ikiisha tunashidwa kumpa mgonjwa huduma hadi pale anapoongezewa damu pia mfano Saratani ya damu inatabia ya kushusha damu sana hivyo tunawaomba watanzania wenzetu wawe wepesi kujitokeza kuchangia damu kwani Kila mmoja akichangia damu anaenda kuokoa maisha ya watu fulani pia damu ni uhai na ukombozi ,pia labda niwashukuru Benki ya damu Tanzania wamekua wakijitahidi sana kukusanya damu kwa ajili ya wagonjwa", alisema Dkt.  Atukuzwe 

Alisema saratani wanazozipokea kwa wingi kwa upande wa watoto saratani ya damu ndio inawakumba sana watoto ,Kwa wanawake saratani ya matiti na Kwa wanaumwa saratani ya tezi dume ndio inawakumba sana wababa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Arusha Women in Business Saccos Ltd Lusinde Urasa alisema kuwa katika kusherehekea siku hii ya wanawake duniani katika chama chao wameona warudishe fadhila zao Kwa wagonjwa wa saratani mbalimbali waliopo katika hospitali ya KCMC ambapo wameamua kuchangia damu wagonjwa wao pamoja na kuwapatia vitu mbalimbali ambavyo walikuwa wakiviitaji.

Alisema tatizo hilo linaonyesha ni kubwa hivyo ni vyema watanzania wakajitoa zaidi ili kuweza kuokoa maisha ya watanzania wenzao ambao wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali ambapo pia wanauhitaji wa damu.

Naye mgeni rasmi  wa maadhimisho hayo Afisa Ushirika mkoa wa Arusha Mkubwa Musa  aliwapongeza wanawake wa chama hicho na kuwaasa waendelee kuwa na moyo huo huo wa kujitoa kwa wenye uhitaji huku akiwasihii kuendelea kuwa waaminifu na wawe wanarejesha vyema fedha ambazo wanachukua katika chama chao ili kuondoa tatizo hilo  kwani wanavyorejesha vyema fedha hizo atapewa mwanamke mwingine na zitaenda kumuinua na atapewa maarifa yatakayo msaidia kiendeleza maisha.

Aidha pia aliwataka  wanawake kutengeneza mipango bila ya kuwa na mipango hawataweza kufikia malengo yao Kama walivyokusudia.

Kwa upande wake meneja wa chama hicho Maria Mange alisema kuwa chama chao kimepata mafanikio ma kubwa tangu kuanzashwa kwani wa sasa wana wanachama 900 wakati walipoanzisha walianza na wanachama 20 ,ambapo pia alisema hadi walishakopeshana zaidi ya shilingi bilioni 20

Alitaja kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu inasema kuwa 'kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu:Jitokeze kuhesabiwa".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com