Basi la Kilimanjaro Express lililopata ajali mkoani Songwe
Watu wanne wamefariki dunia huku wengine 35 wakijeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha basi la Kilimanjaro, linalofanya safari zake kutoka Tunduma kuelekea Dar es Salaam katika mlima Senjele mkoani Songwe.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Rashid Ngonyani, amesema kuwa ajali hiyo imetokea hii leo Machi 14, 2022, ambapo basi hilo lilitumbukia kwenye korongo na kuviringika mara kadhaa.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya Vwawa mkoani Songwe na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu.
Social Plugin