WIZARA YA HABARI YAWAPA MAFUNZO YA MAKOSA YA MTANDAO WAKUU WA UPELELEZI

 

Dkt. Jim Yonazi

Na Dotto Kwilasa,Malunde1 Blog-DODOMA.

WIZARA ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imetoa mafunzo ya makosa ya mtandao (cybercrime) kwa Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na wakuu wa madawati ya makosa ya mtandao wa Mikoa ili kulinda usalama wa raia na nchi kwa ujumla kufuatia kuwepo kwa wimbi la uhalifu wa makosa ya mitandao nchini.

Katiba Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Jim Yonaz, ametoa kauli hiyo leo  jijini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo kwa viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi  kuhusu makosa ya kimtandao huku akiliagiza Jeshi hilo kutoa elimu kwa jamii ili iweze kutambua makosa ya kimtandao na namna ya kuchukua tahadhari ili kujiepusha kushiriki kwenye makosa hayo.

"Nendeni mkatumie upelelezi kutumia mafunzo hayo katika kukabiliana na masuala ya uhalifu wa kimtandao kwa kujifunza zadi ubobezi,dunia inabadilika kuna uhalifu wa kimtandao ambao unapaswa polisi kufuatilia kwa makini na kukabiliana nao,"amesema.

Dk.Yonazi amelitaka jeshi hilo kujifunza mara kwa mara jinsi ya kukabiliana na uhalifu wa kimtandao ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia huku akitolea mfano mgogoro wa Ukraine na Urusi "najua nyie kama askari mnafuatilia kwa makini kabisa kinachoendelea najua mnatambua pamoja na kupigana vita physical lakini kuna vita ya kidigitali,"alisema.

Dkt. Yonazi amefafanua kuwa mafunzo hayo yanawapatia njia ya wapi waelekee hasa kwenye masuala ya usalama wa kimtandao.

Amesema ni vyema kila mmoja anapotoka hapa akumbuke ana wajibu wa kujifunza kila siku, mafunzo hayo ni muhimu sana yameelekezwa kutoonesha njia ya nini tunatakiwa kufanya ili kuhakikisha usalama wa raia unakuwa timamu.

Katibu Mkuu huyo amebainisha kuwa Wizara hiyo ina wajibu wa kuhakikisha usalama katika mtandao unazingatiwa vizuri.


“Mafunzo haya ni endelevu kwa sababu teknolojia zinabadilika, teknolojia za jana na za leo ni tofauti, na zinabadilika kwa maana kwamba speed ya processing inaongezeka mawasiliano yanazidi kuwa haraka, pia namna taarifa zinavyotengenezwa na kuhifadhiwa,”amesema Dk.Yonazi.

Ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo itahakikisha inajenga uwezo wa vifaa, utambuzi, utalaamu ili kufanikiwa kukabiliana na uhalifu wa kimtandao.

Pia amesema kutokana na maisha ya sasa ya sayansi na Teknolojia mafunzo mnayopatiwa ni muhimu, maendeleo ya sayansi na teknolojia, hivyo ni muhimu kwa pamoja mtumie fulsa hii kuwa walimu kwa wenzenu.

Awali Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camilius Wambura, amesema mafunzo hayo yanahusisha washiriki 100 ambao wote ni kutoka kwenye jeshi hilo nchini.

“Ni ukweli usiopingika kwamba teknolojia inabadilika kila kukicha hivyo huhitaji mafunzo ya mara kwa mara kwa watendaji wetu ili kuendana na kasi ya mabadiliko hayo ili kufikia lengo la kupambana na uhalifu huo,”amesema.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa malengo ni kuhakikisha kila siku askari anakuwa na elimu kuhusu makosa ya kimtandao kutokana na kwamba kwasasa uhalifu wote umehamia kwenye eneo hilo.

Awali,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP,Joshua Mwangasa  amesema tayari wameshaanza mradi wa utekelezaji wa kanda sita za maabara za kiuchunguzi ili kupanua wigo wa kiuchunguzi nchini kwani awali walikuwa na maabara moja tu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post