Bernard Maina Mwangi, anayeshtakiwa kwa kukutwa na noti bandia
**
Bernard Maina Mwangi, Katibu Mkuu wa Kanisa Huru la Pentekoste la Afrika (AIPCA) nchini Kenya, ameshtakiwa kwa kumiliki noti bandia za Dola za Kimarekani kiasi cha 365,000 na noti bandia za Kenya kiasi cha shilingi 96,000.
Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Milimani Carolyne Muthoni Njagi amesema kwamba mchungaji huyo amepatikana na pesa hizo ndani ya gari lake wakati akiendesha gari kando ya barabara ya Kiambu ndani ya Kaunti ya Nairobi Machi 10, 2022, mshtakiwa amekiri mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yake na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
"Dereva na gari hilo alisindikizwa hadi makao makuu ya DCI na maafisa wa polisi kwa mahojiano. Upekuaji wa kina wa gari hilo ulifanyika," inasema ripoti ya polisi nchini humo..
Wakati wa kuomba dhamana, mahakama imefahamishwa kwamba Mwangi ni katibu mkuu wa AIPCA. Hakimu amemwachia huru mshtakiwa huyo kwa dhamana ya shilingi za Kenya 100,000.