Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Khadija Issa Said(wapili kulia) akiwasha kifaa maalum kuashiria uzinduzi huo. (Kutoka kushoto wa pili )Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Alliance ,Krinshnan Anantha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Axieva,Gaurav Dhingra na Mkurugenzi wa Airtel Money wa kampuni ya Airtel Tanzania Isack Nchunda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Alliance ,Krinshnan Anantha (katikati) akibadilishana mawazo na Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Khadija Issa Said (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya Bima hiyo na Aitel uliofanyika jijini Dar es Salaam Kushoto ni Mkurugenzi wa Axeiva,Gaurav Dhingra.
Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Khadija Issa Said(wapili kulia) akibadilishana mawazo na watendaji Waandamizi wa makampuni yaliyoshirikiana kuwezesha kupatikana huduma za bima kidigitali wakati wa hafla ya uzinduzi ambao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Alliance ,Krinshnan Anantha (wapili kushoto) Kushoto ni Mkurugenzi wa Axeiva, Gaurav Dhingra na Mkurugenzi wa Aitel Money Isack Nchunda.
Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Khadija Issa Said katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni zilizoingia kwenye ushirikiano wa kuzindua huduma za bima za kidigitali wakati wa hafla ya uzinduzi.
****
Wateja wa kampuni ya Alliance Insurance, sasa wanaweza kupata huduma za bima kwa magari binafsi na biashara kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi kutokana na ushirikiano wa makampuni ya Alliance Insurance Corporation, Airtel Money Ltd na mtoa huduma wa teknolojia ya BIMA Axieva Africa Lab.
Kupitia huduma inayojulikana kama AIRTEL BIMA itasaidia wateja kuepuka usumbufu wa kutembea safari ndefu, usumbufu wa kutembea na fedha taslimu na changamoto ya kubeba makaratasi kutafuta huduma za bima kwa ajili ya magari yao badala yake wanaweza kupiga*150*60# kwenye simu zao za Airtel muda wowote na kupata menu ya BIMA inayotolewa na kampuni ya bima ya Alliance papo hapo ikiwa chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini-TIRA, kampuni ya Alliance inaongoza kwa kutoa huduma za bima za magari.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua ushirikiano huo mpya, Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Hadija Issa Said ameyapongeza makampuni yaliyoshirikiana kuzindua mpango huo.
“Nachukua fursa hii kupongeza timu ya wafanyakazi wa Airtel, Alliance na Axieva kwa jitihada zao mpaka kufanikisha uzinduzi wa huduma hii ambayo imelenga kuleta mapinduzi kuwezesha kupatikana huduma za Bima kwa njia kidigitali.Huduma hii itawezesha idadi kubwa ya Watanzania kupata huduma za bima wakati wowote, mahali popote kupitia simu zao za mkononi”
Hakika Alliance na Axieva mmefanya kazi nzuri sana na Airtel katika kufikia hatua muhimu kwa Sekta hii” alisema Khadija Issa Said.
Anantha Krishnan, Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Alliance Insurance Corporation alisema, "Uzinduzi wa leo na Airtel na Axieva ni matokeo ya dira ya pamoja ya Alliance ya mabadiliko ya sekta na upatikanaji wa kidijitali kwa kila mtumiaji.
Imekuwa ni dhamira yetu kuwaweka wateja wetu kwanza, na kuwaletea ubunifu wa huduma mpya na bora zenye kurahisisha maisha.. Tunaamini kwamba uzinduzi huu wa USSD kama njia ya usambazaji wa huduma zetu utaongeza thamani kubwa kwa Wateja wetu, Alliance, Sekta na Nchi.
Hakika hii ni siku ya Kihistoria! Na tunajivunia kwamba kwa ruhusa kutoka TIRA,inayodhibiti na kusimamia dira kisekta, tunapeleka huduma za Bima kwa pamoja katika hatua mpya, ambapo nchi nyingine zitapata fursa ya kujifunza kutoka Tanzania” alisema Krishnan.
Ushirikiano kati ya Airtel, Alliance na Axieva unategemea kazi ya Axieva ambayo imekuwa ikifanya katika ngazi ya kimataifa ya kufanikisha ujumuishaji wa kifedha na kubuni mbinu za kufanikisha huduma upatikanaji wa huduma za kifedha
Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money wa Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema , “Tunayo furaha kuleta mageuzi haya kabambe ya Airtel Money BIMA kidigitali kwa kupitia ubinufu tulio nao kupitia Airtel,niwahakikishie wateja wetu kuwa ushirikiano huu na Axieva pamoja na Alliance Insurance wa kuleta huduma za bima kidigitali ni mwanzo wa hatua kubwa wa kuja na huduma nzuri zaidi hapa.
Huduma za bima hadi sasa imesalia kuwa mojawapo ya huduma ambazo hazipewi kipaumbele kutokana na hali ya mlolongo mrefu ya upatikanaji wake,na malipo ya huduma hii nyingi hutumia makaratasi.Hivyo kwa kutumia huduma ya Airtel Money pamoja na ushirikiano huu wa miundombinu,tunaondoa vikwazo vyote hivi kwa wateja wetu na kuweawezesha kupata huduma za bima kwa kugusa kitufe tu.
Nia yetu ni kuhakikisha Watanzania wote milioni 60 wanapata huduma za Airtel BIMA ili waishi maisha huru.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Axieva Afrika, kampuni inayoendesha teknolojia na ushirikiano wa Axieva BIMA alisema “Dhamira yetu katika AXIEVA ni kuunda mifumo ikolojia endelevu; ambayo inaweza kuathiri vyema na kuwezesha jumuiya za wenyeji kupitia matumizi ya teknolojia. Axieva BIMA ni mfano mmoja tu wa jinsi mnyororo mzima wa thamani wa tasnia changamano unavyoweza kubadilishwa kidijitali ili kufungua, ufikiaji, utoaji, kiwango na ufanisi wa kifedha kwa Mamilioni.
Kwenye jukwaa la Airtel BIMA, hakuna haja ya kujisajili au kujisajili mapema. Mtumiaji anaweza tu kupiga *150*60# na kufuata menyu iliyo chini ya Airtel Money Financial Services ili kupata Bima ya Magari iliyothibitishwa na TIRA kwa Magari, Baiskeli au Bajaj zao” alisema Dhingra.
Social Plugin