Msanii maarufu wa filamu nchini na mchekeshaji, Steve Mengere maarufu Steve Nyerere, ambaye alikuwa ameteuliwa kuwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania(SMT), ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Ijumaa Machi 25, 2022 ikiwa ni siku chache baada ya baadhi ya wasanii kudai kuwa hana sifa za kuliongoza Shirikisho hilo.
Aidha, Steve ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Rais na shirikisho hilo wakati wote.
“Nimejiuzulu niendelee na kazi nyingine za msingi, na hii sio kwamba haikuwa kazi ya ms ngi. Nipo katika maisha yao, sitaki kutoka katika maisha yao, mimi sijui kesho yangu itakuwaje.
“Nimejiuzulu kwa sababu sioni kama hizi kelele zina tija kwa Taifa, ya nini.. ya nini …ya nini mie? Nimeachia. Taifa letu lina mambo ya msingi na makubwa kumsapoti Rais Samia.
“Tunapambana na mama na mtoto, stiglers Gorge, madarasa na mambo mengine mengi, halafu tena tugombanie usemaji? Cheo ambacho hata mshahara wake siuoni?” amesema Steve Nyerere.
Social Plugin