Naibu waziri wa ulinzi wa Urusi Alexander Fomin anasema Urusi itapunguza kwa kiasi kikubwa shughuli za kijeshi nje ya Kyiv na Chernihiv – hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Tass.
Vikosi vya Urusi vinaonekana kukwama katika eneo hili – hapo awali wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema kwamba vikosi vya Ukraine vilifanikiwa kuwarudisha nyuma Warusi kutoka nafasi kadhaa.
Ilisema Urusi ilisalia kuwa tishio kubwa kwa Kyiv kutokana na uwezo wake wa kushambulia.
Mji wa kaskazini uliozingirwa wa Chernihiv umesalia chini ya mashambulizi ya Urusi leo, kulingana na maafisa wa Ukraine.
Meya wa jiji hilo anakadiria kuwa wakaazi 400 wameuawa hapo tangu vita kuanza.
Alexander Fomin alisema uamuzi wa “kupunguza kwa kiasi kikubwa” shughuli za kijeshi za Urusi katika miji hiyo miwili ulichukuliwa ili “kuongeza uaminifu wa pande zote” na kusaidia kusababisha mazungumzo zaidi na kufikia “lengo la mwisho” la makubaliano yaliyotiwa saini kati ya pande hizo mbili. maoni yaliyoripotiwa na shirika la habari la Urusi Ria Novosti.
Kutokana na ukweli kwamba mazungumzo juu ya makubaliano ya kutoegemea upande wowote Ukraine na hali isiyo ya nyuklia na dhamana ya usalama (kwa Ukraine) yanaingia katika hatua ya vitendo, na kwa kuzingatia kanuni zilizojadiliwa wakati wa mkutano wa leo, Wizara ya Ulinzi ya Shirikisho la Urusi imechukua uamuzi wa kupunguza kwa kiasi kikubwa shughuli za mapigano katika maeneo ya Kyiv na Chernihiv ili kuongeza kuaminiana na kuunda mazingira muhimu kwa mazungumzo zaidi na kusainiwa kwa makubaliano yaliyotajwa hapo juu.
Alexander Fomin
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi