*****
Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog-DODOMA
Hatua hiyo imekuja kutokana na kuonekana kwa tovuti yenye jina la https://www.sensatanzania.com ambayo inatangaza kuwepo kwa nafasi za kazi za makarani wa sensa na tayari baadhi ya watu wameshajisajili kwenye mfumo huo kwa malipo.
Tahadhari hiyo ilitolewa jijini hapa leo na Mtakwimu Mkuu wa Serikali,Dkt.Albina Chuwa wakati akiongea na Waandishi wa habari kuhusu taarifa hiyo ambapo aliwata ka wananchi kutambua kua Serikali haijaanzisha tovuti rasmi ya sensa hivyo tovuti hiyo si rasmi na haitambuliwi na Serikali.
"Nafasi za Ukarani na usimamizi wa sensa zitatangazwa rasmi kupitia tovuti mitandao ya kijamii ya NBS na OCGS,Radio,runinga na magazeti mara baada ya taratibu zote za Serikali zitakapokamilika,"amesema.
Amesema kazi ya kuwapata watumishi hao wa sensa itasimamiwa na kamati za sensa za Mkoa ambazo wenyeviti wake ni wakuu wa mikoa husika.
"Nia ya serikali kufanya hivyo ni kuhakikisha watu wote wanaotaka kufanya kazi za ukarani na usimamizi wa sensa watoke katika maeneo yao wanayoishi,"amesema.
Dkt.Chuwa amesema hadi sasa Ofisi imeshatoa taarifa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)ili wachukue hatua za haraka kuwabaini matapeli wa aina hiyo.
Social Plugin