Wafanyakazi wa Shirika la RAFIKI SDO na Wafanyakazi wa Kujitolea (Volunteers) wa Mradi wa EPIC unaolenga Kupunguza Maambukizi Mapya ya Virusi vya UKIMWI katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga wamefanya sherehe ya kupongezana kutokana na kazi nzuri wanayofanya katika jamii.
Sherehe hiyo imefanyika usiku wa leo Ijumaa Machi 25,2022 katika Ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa pia na wafanyakazi wa RAFIKI SDO kutoka mikoa ya Shinyanga, Geita na Mara.
Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a amesema Sherehe hiyo ambayo imehudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura imekutanisha pamoja wafanyakazi wa RAFIKI SDO kuanzia ngazi ya kata hadi taifa kwa lengo la kula na kunywa pamoja na kusherehekea mafanikio mbalimbali ya Shirika hilo.
"Nyinyi Waelimisha rika mnafanya kazi nzuri sana, bila nyingi Rafiki SDO si lolote..Naomba mfanye kazi zenu kwa uaminifu, msidanganye kwenye Data/Takwimu, leteni taarifa zilizo sahihi. Hakikisheni mnafanya kazi kwa weledi mkubwa, shirikianeni na changamoto zikitokea zimalizeni",amesema Ng'ong'a.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura amesema majukumu mengi yanayotekelezwa na RAFIKI SDO yanapaswa kufanywa na serikali lakini wanafanya hayo kwa kushirikiana na serikali.
"Kutokana na kazi nzuri ya asasi za kiraia ndiyo maana serikali imekubali kushirikiana na NGO,s. Wajibu wetu ni kutambua mchango unaofanywa na asasi za kiraia. Tunawashukuruni sana RAFIKI SDO kwa kazi nzuri mnayoendelea kufanya.
Kutokana na kazi nzuri Manispaa ya Shinyanga inawapatia Kiwanja eneo la Ibadakuli ili mjenge ofisi yenu kwa sababu kazi mnazofanya wanufaika wakubwa ni wananchi ",amesema Satura.
Tazama Video wafanyakazi Rafiki SDO wakicheza muziki
Mwandishi Mkuu wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ametusogezea picha za matukio mbalimbali yaliyojiri..Tazama Hapa chini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza kwenye sherehe ya Wafanyakazi wa Shirika la RAFIKI SDO. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza kwenye sherehe ya Wafanyakazi wa Shirika la RAFIKI SDO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza kwenye sherehe ya Wafanyakazi wa Shirika la RAFIKI SDO
Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la RAFIKI SDO, Happiness Misael akizungumza kwenye sherehe hiyo.

Zoezi la Kukata Keki likiendelea kwenye sherehe hiyo.
Zoezi la Kukata Keki likiendelea kwenye sherehe hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la RAFIKI SDO, Happiness Misael akikata keki
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la RAFIKI SDO, Happiness Misael akikata keki
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Soma pia:
Tazama Video wafanyakazi Rafiki SDO wakicheza muziki
Social Plugin