Watu watatu wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori la mizigo lenye namba za usajili T 947 BQB kuacha njia kisha kuparamia nyumba eneo la Mikumi, Barabara Kuu ya Morogoro – Iringa.
Kwa mujibu wa majeruhi wa ajali hiyo, Rajabu Kapombe amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 alfajili ya leo Ijumaa, Machi 25, 2022 mara baada ya lori hilo kufeli breki na kupoteza muelekeo kisha mtu mmoja aliyekuwa pembezoni mwa barabara kabla ya kuparamia nyumba hiyo.
Akizungumzia ajali hiyo, mganga wa zamu wa Hospital ya St Kizito, Dk. Simon Veda amethibitisha kupokea miili ya watu watatu akiwemo dereva wa lori hilo, abiria mmoja pamoja mtembea kwa miguu huku majeruhi akiendelea kupatiwa matibabu katika hoapital hiyo.
Social Plugin