HAWA NDIYO WANAFUNZI 10 BORA MATOKEO MTIHANI WA DARASA LA NANE (KCPE) MWAKA 2021

Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) ya mwaka 2021 hatimaye yametangazwa takriban wiki tatu baada ya watahiniwa kumaliza mtihani huo.

Matokeo hayo yametolewa na Waziri wa Elimu nchini Kenya Profesa George Magoha katika makao makuu ya Baraza la Kitaifa la Mitihani Nchini (KNEC) Mitihani House jijini Nairobi. Mwanafunzi wa Gilgil Hills Academy Magata Bruce Mckenzie aliibuka nambari moja katika matokeo ya mtihani huo yaliyotolewa adhuhuri ya Jumatatu, Machi 28.

Magata amepata alama 428, ikiwa ni upungufu wa alama saba ikilinganishwa na mwanafunzi aliyeongoza katika matokeo ya mtihani wa KCPE mwaka 2020 ambaye alipata alama 433. Magoha vilevile alitangaza kuwa kulikuwa tu na tofauti ya alama tatu kati ya mtahiniwa aliyeibuka wa kwanza na ule aliyenyakua nafasi ya 14 kwa alama 425.

Hii ni orodha kamili ya wanafunzi kumi bora katika mtihani wa KCPE 2021: 

1. Magata Bruce Mckenzie - Gilgil Hills Academy - alama 428
 2. Momanyi Ashley Kerubo - Makini School - alama 427 
3. Kwoma Charity Buyanzi -Holy Family Misikhu Girls Primary School- alama 426 
4. Mbugua Sharon Wairimu - Emmanuel Academy - alama 426 
5.Muteti Shantel Ndinda - Kitengela International School - alama 426
 6. Stanley Otieno Omondi - Rofin Field Junior School - alama 426

7. Wekesa Naomi - Whitestar Academy - alama 426 
8. Kimani Ethan Karuga - Stepping Stones Preparatory - alama 426
 9. Njeru Joel Junior - Nyagwa Primary - alama 425 
10. Muriuki Victor - PCEA Mwimbi Boarding Primary school - alama 425
 11. Diana Rose Natola - Fesbeth Kakamega - alama 425
 12. Kaderia Emmanuel Munene - New Bambini - alama 425 
13. Emmanuel Kiplagat Ngetich - Moi Kabarak - alama 425
14. George Morris Otieno - Hill School - alama 425

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم